Hey Pressto Conference 2021

Just another My Sites site

Kiswahili

Hey Pressto! ni kongamano la ClassicPress na WordPress linaloandaliwa kwenye Twitter.

Mawasilisho ya Hey Pressto! yana hadi twiti 15, moja ikichapishwa kwa kila dakika.

Hey Pressto! inatia moyo na inalenga kuwa kongamano linalofikiwa zaidi tunaloweza kuwa. Iwapo unaweza kuona njia tunazoweza kuboresha kile ambacho tunafanya, tafadhali tufahamishe.

Hey Pressto! ingependa kuskia kuhusu tovuti yako au uzoefu wako. Je, una tovuti iliyo na machapisho milioni moja? Ajabu, tafadhali tuambie zaidi. Je, una tovuti iliyo na chapisho moja bora? Ajabu, tafadhali tuambie zaidi! Je, ulichapisha chapisho lako la kwanza? Hiyo ni ajabu, pia! Tafadhali tuambie zaidi! Iwapo umefanya kitu chochote. Hiyo ni ajabu! Tafadhali tuambie zaidi!

Hey Pressto! ni ya watu wanaotumia ClassicPress au WordPress kufanya chochote. Ni ya wasanidi wanaowezesha vitu vya ajabu, kwa watu wanaoendesha mikutano na matukio, kwa watu wanaojali utawala. Lakini zaidi ya kitu chochote, ni yako.

Hey Pressto! Inafahamu vyema kwamba tunaishi katika ulimwengu wenye ufundi mwingi usio sawa, na hatuwezi kuurekebisha sisi wenyewe. Tunataka kuwa tukio linalosherehekea maarifa kutoka kwa maeneo yasiyowakilishwa ipasavyo na sauti zinazopuuzwa.

Hey Pressto! inaendeshwa kwa saa 12, hivyo utakuwa na baadhi ya muda wa kujiunga na kuwasilisha popote ulipo ulimwenguni.

Hey Pressto! inakaribisha mawasilisho katika lugha yoyote.

Hey Pressto! inajua kwamba Twitter si pahali bora kwa kila mmoja, na tuna akaunti zisizotambuliwa za watu kuwasilisha nazo iwapo wanapendelea.

Hey Pressto! ina huduma ya ushauri ya bila malipo na isiyotambuliwa unayoweza kutumia iwapo ungetaka baadhi ya usaidizi wa kuandaa mawasilisho yako.

Mawasilisho ya Hey Pressto! yana urefu wa vibambo 280 – sawa tu na twiti moja.

Hey Pressto! ingependa utembelee ukurasa wetu wa mawasilisho (https://2020.heypresstoconf.org/submit/ ). Acha tuone iwapo tunaweza kukusaidia kushiriki uzoefu, maarifa na hadithi yako.

Hey Pressto! ina matumaini kwamba utajiunga nasi.

Hey Pressto! ina matumaini kwamba utaambia marafiki zako kuhusu Hey Pressto!

 

Hey Pressto! inakushukuru kwa kusoma hili. Jitunze na uwe na siku njema.

Hey Pressto Conference 2021